Ally Masoud 'Kipanya'

Ninayo heshima kubwa kuwatumikia kama Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania (TASSIM). Ni furaha na faraja kubwa kukutana na wanachama na viongozi wengi nchini kwetu na kuona jinsi Kamati ya Utekelezaji na Sekretarieti yetu pamoja na wafanyakazi wake wanavyoweza kuwahudumia vyema kama sauti ya wenye viwanda vidogo na vya kati pamoja na wazalishaji wadogo Tanzania.

Kutokana na uzoefu wangu wa takribani miaka 30 kwenye sekta binafsi kabla ya hii, nimejizatiti kuhakikisha kuwa wanachama wetu wanapata kuona thamani ya moja kwa moja kutoka kwenye uanachama wao. Dhamira yetu ni kutoa jukwaa, mtandao, maudhui, uwakilishi na usemaji utakaokuza uwezo wako wa kuendeleza biashara yako.

TASSIM ina heshima na bahati kubwa ya kuwa na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson Mwansasu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mshauri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji Waziri wa Viwanda na Biashara kama Mlezi wetu. Tunatambua umuhimu wa ushirikiano na mshikamano na viongozi wa ngazi za juu kwenye kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Kama Mwenyekiti, nitadumisha ushirika baina ya sekta tofauti na harakati za pamoja zinazosaidia ukuaji wa uvumbuzi, vipaji na biashara. Bila shaka, tukiwa na mtazamo huu wa ushirikiano hii itapelekea kuongeza maendeleo jumuishi yatakayopelekea nchi nchi yetu kwenye ustawi pia.

Ni matumaini yangu tufanye kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunaweka Chama kwenye mlengo wa kuwa chombo kilichoiva sio tu mawazo ya biashara bali hata ya uongozi, pia kuwa chombo cha ushirikiano na kinara kwenye uwakilishi na utetezi wa viwanda vidogo na vya kati ndani ya Tanzania. 

Nina imani kila kitu kina mchango wake katika kusaidia ukuaji wa viwanda vidogo na vya kati ambavyo vinachangia ustawi wa nchi yetu. Uwepo na uhusiano wetu na viwanda vidogo na wazalishaji wadogo kunaruhusu sisi kuonesha umuhimu wetu kwa ngazi zote nchini Tanzania.

Mwisho, nakukaribisha kujiunga na kushiriki na Chama cha Wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania (TASSIM). Pamoja, tuutumie uwezo na rasilimali zetu kikamilifu kwenye viwanda vyetu ili tuweze kujenga mahusiano ya kudumu. 

Tafadhali waweza kuwasiliana nami kupitia info@tassim.or.tz kwa mawazo au mapendekezo. Mchango wako ni muhimu sana kwetu na nina shauku ya kusikiliza na kujifunza kutoka kwako.

Kila la Kheri!