Chama cha wenye Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania (TASSIM) ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa kwa lengo la kuunda jukwaa na mifumo kwa ajili ya kusaidia na kukuza ukuaji katika sekta ya viwanda vidogo na uzalishaji Tanzania.

Hivyo, TASSIM ni shirika lililopatikana kwenye misingi ya kusaidia na kuwezesha biashara ndogo na za kati haswa wazalishaji wa viwanda vidogo vya Tanzania kwa maendeleo na ukuaji wa kiuchumi. TASSIM imeundwa kutokana na ufahamu kwamba kulikuwa na pengo katika uwakilishi na usaidizi wa biashara za kitaalamu za viwanda vidogo na vya kati ambavyo vinataka kukua na kuwa biashara kubwa.