Kikao hiki cha tatu, kiliweza kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa sekta binafsi na taasisi za kifedha za hapa nchini pamoja na wamiliki wa Viwanda vidogo na wazalishaji wadogo wa Tanzania, ambao ni wanachama wa TASSIM walioshiriki kwa niaba ya wanachama wote nchini. Kikao hiki cha kimkakati ambacho malengo yake makuu, ni pamoja na kuangalia maeneo ambayo Shirika la MCC linaweza kujikita katika kusaidia kutokomeza umaskini kupitia uwezeshaji hasa uliojikita katika uzalishaji wa vitu mbalimbali.

Mwakilishi wa Shirika hilo la MCC kutoka Washington, Marekani, akikieleza kikao hicho, alidai kuwa katika mpango huu wa kwanza, wamtenga kati ya dollar za Kimarekani million 20, 000,0000 hadi 60,000,000 zinazotarajiwa kutumika katika kuondoa umaskini na kuinua kazi za wafanyabiashara hawa.

Katika majumuisho ya mijadala yote hiyo, ilionekana kuwa upo umuhimu wa kuwajengea uwezo wa elimu ya biashara na pia kuona namna ambavyo wanaweza kuwa maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao za uzalishaji (Business Parks) kwani kufanya hivyo kutarahisisha kufikiwa na kupata elimu kwa pamoja.