Kama mwakilishi wa wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania, majukumu makubwa ya TASSIM ni pamoja na kutoa ushauri na mapendekezo ya maboresho ya sera na utungwaji wa sera mpya pamoja na usimamizi wa utekelezaji wa sera hizo ili kuwezesha ukuaji na uzalishaji wa viwanda vidogo na vya kati nchini Tanzania.