Ninayo heshima kubwa kuwatumikia kama Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania (TASSIM). Ni furaha na faraja kubwa kukutana na wanachama na viongozi wengi nchini kwetu.
TASSIM ni shirika linalosimama kama wawakilishi wa wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania. TASSIM inatekeleza jukumu la kuunganisha na kushirikiana na serikali na taasisi husika katika kuhakikisha mawazo na changamoto za wanachama wake zinapata uvumbuzi kwa lengo la kukuza sekta ya viwanda nchini Tanzania.
Ninayo heshima kubwa kuwatumikia kama Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania (TASSIM). Ni furaha na faraja kubwa kukutana na wanachama na viongozi wengi nchini kwetu.
Kama mwakilishi wa wamiliki wa Viwanda Vidogo na Wazalishaji Wadogo Tanzania, majukumu makubwa ya TASSIM ni pamoja na kutoa ushauri na mapendekezo ya maboresho ya sera na utungwaji wa sera mpya pamoja na usimamizi wa utekelezaji wa sera hizo ili kuwezesha ukuaji na uzalishaji wa viwanda vidogo na vya kati nchini Tanzania.