Uanachama umewekwa wazi kwa watu wote wenye viwanda vidogo na wazalishaji wote pamoja na wadau wanaojihusisha na kuunga mkono sekta hiyo kwa namna mbalimbali. TASSIM ina makundi manane ya uanachama ambayo ni wanachama wa kawaida (watu binafsi), Makampuni Madogo, Mashirika na Makundi ya Uzalishaji, Mwanachama Mshirika, Mwanachama Mtaalamu, Mwanachama Mwanafunzi, Mwanachama Diaspora, ambao uanachama wao utaidhinishwa na uongozi kama inavyoelekeza katiba ya TASSIM.

Mtu yeyote atakayetamani kuwa mwanachama wa TASSIM atatuma maombi yake kwa Katibu Mkuu wa TASSIM na maombi hayo yatafanywa mapitio na uongozi; ili kuweza kukubalika kuwa mwanachama.