- Kuhudhuria Mkutano Mkuu na Mikutano mingine itakayoitishwa na TASSIM.
- Kuomba na kupata taarifa muhimu kutoka TASSIM.
- Kupata majarida na habari zinginezo zinazotolewa na TASSIM.
- Upatikanaji wa rasilimali muhimu ambazo zitatolewa na TASSIM.
- Haki ya kupiga na kupigiwa kura.
- Haki ya kupewa kipaumbele cha kuwa mshauri kwenye mikataba ya TASSIM kulingana na vigezo na masharti ya TASSIM.
- Kupewa kipaumbele cha kushiriki kwenye mikutano na majukwaa ya kimkakati yaliyoandaliwa na taasisi zingine kama mwakilishi kutoka TASSIM.
- Kupata kipaumbele cha kushiriki kwenye kamati za ufundi.
- Kupata punguzo la asilimia 20% kwenye ada ya usajili wa kozi, semina, mikutano na majukwaa yanayoandaliwa na TASSIM.