- Kuunganisha viwanda vidogo na wazalishaji katika jitihada za kuunda jukwaa la kubadilishana mawazo na uzoefu kupitia mikutano, warsha, maonesho na kozi rasmi.
- Kuweka jukwaa la sauti ya pamoja kwa wasio na sauti katika sekta muhimu ya uchumi ambayo imeachwa nyuma kwa miaka mingi.
- Kusaidia ukuaji wa sekta ya viwanda vidogo kwa sauti moja na imara.
- Kupitia sauti moja inayolenga kurahisisha uhusiano kati ya Serikali, Taasisi za umma na binafsi, na wadau wa kimataifa, Chama kitalenga;
- Kuwa kiungo cha utoaji ushauri na mapendekezo juu ya sera au masuala ya kitaifa yanayohusiana na wazalishaji wa viwanda vidogo.
- Kushirikiana na Serikali au taasisi nyingine yoyote ya kitaifa au kimataifa katika kukuza ukuaji wa viwanda vidogo.
- Kuanzisha na kukuza uhusiano wa kazi na mashirika au taasisi za kitaifa na kimataifa yenye malengo sawa.
- Kutumika kama jukwaa la majadiliano ya kitaifa na kimataifa juu ya ajenda ya serikali, ya dunia au ajenda yoyote husika.
- Kwa kushirikiana na Serikali au chombo chochote kingine cha kitaifa au kimataifa katika kuandaa semina, warsha, mikutano juu ya mada yoyote inayohusiana na Viwanda Vidogo.
- Kushirikiana na wawekezaji wa kigeni, makampuni ya kimataifa kusaidia na kuwekeza kwenye viwanda vidogo.
- Kuchapisha majarida, magazeti na vipeperushi kama njia ya mawasiliano na usambazaji wa taarifa sahihi.